July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amtembelea Mkurugenzi LHRC

Spread the love

RAIS wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Aga Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Kijo-Bisimba alipata ajali mbaya ya gari jana katika daraja la Salender Dar es Salaam jana.

Katika ajali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba amedaiwa kuvunjika mguu mmoja baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kupinduka mara nne.

Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi wakati akitoka kusali eneo la Posta akitumia gari dogo ya Toyota Prado yenye namba za usajili T159 ATY.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa LHRC, Ezekiel Masanja alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo alikwenda na kumchukua Dk. Kijo-Bisimba.

Amesema alimpeleka katika Hospitali ya Agha Khan kwa   matibabu.

Kwa mujibu wa Masanja, vipimo vya awali vilionyesha amevunjika mguu lakini hadi jana jioni madaktari walikuwa wakiendelea kumuangalia zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alikiri kutokea tukio hilo akisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.

“Sina maelezo yanayojitokeza kuhusu ajali hii kwa sababu askari wanaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo chake,” amesema Wambura.

Mashuhuda wamesema gari la Dk. Kijo-Bisimba liligongwa   ubavuni na gari nyingine iliyokuwa inatoka eneo la Sea View kwenda barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Wamesema gari hilo lilikuwa linaendeshwa na kijana ambaye hakufahamika na baada ya kuligonga gari la Kijo-Bisimba lilizunguka mara nne na kupinduka.

Katika gari la Dk. Kijo-Bisimba walikuwamo watu wawili na inadaiwa gari lililomgonga lilikuwa likiendeshwa na kijana wa miaka 13.

error: Content is protected !!