June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ampa shavu Pinda

Spread the love
RAIS John Magufuli amemteua Mizongo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), anaandika Pendo Omary.
Taarifa ya uteuzi wa Pinda imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Gerson Msigwa, Kaimu Mkuu wa Mawasiliano, Ikulu.
Sehemu ya taarifa hiyo inasema “Mizengo Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha –Rose Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.”
Tangu atupwe nje katika hatua ya awali ya mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, Pinda amekuwa kimya katika masuala ya siasa.
error: Content is protected !!