RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imemnukuu, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akiwataja walioteuliwa.
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Dk. Shein anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Barnabas Samatta ambaye anamaliza muda wake.

Pili, Rais Magufuli amemteua Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Dk. Mwakyembe aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, anachukua nafasi ya Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Gaudentia Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Gaudensia ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Balozi Kijazi amesema, uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Jumanne tarehe 24 Novemba, 2020.
Leave a comment