May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amlilia Maalim Seif

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliywekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Maalim Seif (77), amekutwa na mauti, majira ya saa 5.00 asubuhi leo Jumatano, tarehe 17 Februari 2021, wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa za kifo cha kiongozi huyo shupavu nchini, zimetangazwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.

Akitangaza msiba huo mkubwa kwa taifa, Dk. Mwinyi amesema, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, imempoteza kiongozi shupavu, jasiri na mkweli. Ametangaza siku saba za maombolezo.

Maalim Seif alikuwa katika Muhimbili, kwa ajili ya matibabu, tangu 9 Februari mwaka huu.

Katika salamu zake hizo, Rais Magufuli, ameeleza kupitia ukurasa wake wa Twitter, “nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.”

“Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Dk. Mwinyi, familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amuweke mahali pema peponi. Amina.”

error: Content is protected !!