June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amlilia Jumbe

Spread the love

DK. John Magufuli rais wa Tanzania ametuma salamu za rambirambi kwa Ally Mohamed Shein, rais wa Zanzibar kufuatia kifo cha Aboud Jumbe, aliyekua rais wa awamu ya pili Zanzibar, anaandika Hamisi Mguta.

Jumbe amefariki dunia leo nyumbani kwake Mjimwema Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Magufuli amesema Tanzania imepoteza mtu muhimu ambaye alipigania na kuijenga Tanzania tunayoiona leo.

“Kupitia kwako rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi napenda kuwapa pole familia ya Marehemu, Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wananchi wote na Watanzania kwa ujumla kwa kufikwa na msiba huu Mkubwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Kiongozi huyo ambaye baada ya kuuawa kwa Rais Abeid Karume aliamua kujiuzulu nafasi ya urais wa Zanzibar kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni kuhitilafiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa wakati huo.

Hata baada ya kujiuzulu nafasi yake ya urais Jumbe hakuwa akionekana wala kualikwa au kuhudhuria katika shughuli mbalimbali za chama wala za Serikali jambo lililokuwa likizua sintofahamu zaidi.

error: Content is protected !!