July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amkaba mkoa meneja TBA

Waziri wa Ujenzi, John Magufuri

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ameagiza aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Ndossa kusimamishwa kazi mahali alipo ili arejee kujibu tuhuma na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria. Anaadika Mwandishi wetu … (endelea).

Pia, waziri Magufuli ametoa siku 14, kwa TBA, kuanza ukarabati wa ofisi za wakuu wa wilaya za Siha na Moshi baada ya kubainika majengo hayo yamejengwa chini ya kiwango.

Ametoa alitoa agizo hilo wakati akikagua jengo la mkuu wa Wilaya ya Siha baada ya kupewa taarifa za jengo hilo kujengwa chini ya kiwango, hali iliyosababisha shughuli za mkuu wa wilaya kuhamishiwa kwenye ofisi za maji za halmashauri hiyo.

Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga amemweleza waziri kuwa wanasikitishwa na kasoro za kiufundi zilizojitokeza katika jengo hilo na kwamba watawachukulia hatua wote waliohusika katika kuchangia majengo hayo kuwa chini ya kiwango.

Mwakalinga amesema tayari TBA imefanya tathmini ya gharama za ukarabati wa jengo la wilaya ya Siha ambao utafanyika katika kipindi cha wiki 18 na kugharimu sh. milioni 50.

Majengo ya ofisi za wakuu wa wilaya za Siha na Moshi yamejengwa kwa usimamizi wa TBA ambapo wahusika walishindwa kuyatumia wakihofia usalama wao baada ya kuona dosari.

error: Content is protected !!