September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli amchagua tena Samia mgombea mweza

Spread the love

RAIS John Pombe Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, kuwa mgombea wa Urais wa Tanzania, kwa asilimia 100 leo Jumamosi tarehe 11 Julai 2020.

Mwenyekiti huyo wa CCM amesema, ameamua kumchagua mara ya pili Samia kwa kuwa ana heshima pamoja na kutekeleza maagizo yake.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Rais Magufuli alimchagua Mama Samia kuwa mgombea mweza.

“Nataka niseme kwa dhati bila unafiki, nilipomchagua Mama Samia kuwa mgombea mwenza mwaka 2015,  sikujua vizuri uchapakazi wake wakati ule.  Lakini mama huyu nasema kwa dhati bila unafiki ni mchapakazi ana heshima kila nikimtuma anaenda,” amesema Rais Magufuli.

Awali, Rais Magufuli alisema katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitaka kumchagua Dk. Hussein Mwinyi, kuwa mgombea mwenza wake, lakini alimpendekeza Mama Samia, kwa kuwa mwanamke ana ushawishi katika jamii.

“Nataka niwape siri moja ambayo sikutaka kuwapa hapa na sikutakiwa kuisema hapa, lakini leo naisema, wakati nachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM niliowachagua wawe wagombea wenza alikuwa Mwinyi na Mama Samia, huo ndio ukweli,”  amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Mama Samia asingekuwa mwanamama, makamo wa rais alikuwa ni Mwinyi, Mzee Jakaya Kikwete anafahamu wote hawa wanafahamau, lakini muelewe ukishindanishwa na mama utashindwa tu, na wa kina mama siku zote wanatushinda sisi wanaume, wanatushinda kwa mambo mengi,” amesema

Rais Magufuli alikuwa anasema hivyo wakati akimzungumzia Dk. Mwinyi kwa utulivu na kutokubweteka kwa kuwa ni mtoto wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Dk. Mwinyi amepitishwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 akipigania kumrithi Rais Ali Mohamed Shein ambaye anamaliza muhula wake wa miaka kumi.

error: Content is protected !!