August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli ambabua Kikwete hadharani

Spread the love

RAIS John Magufuli amemwambia Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwamba ‘umeniachia mizigo’, anaandika Charles William.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo mbele ya Rais Kikwete kwamba, serikali yake (ya awamu ya tano) inakabiliana na ‘mizigo’ aliyoiacha Rais Kikwete katika utawala wake.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameeleza kushangazwa kwake na namna taratibu za uendeshaji wa nchi katika sekta mbalimbali ulivyovurugwa na kuharibiwa chini ya utawala Kikwete.

Amesema hayo mbele ya Kikwete leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alipohutubia wanafunzi wa chuo hicho baada ya kumaliza shughuli kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa utakaogharimu zaidi ya Dola za Marekani 40 milioni.

Katika hotuba yake kwa wanafunzi wa chuo hicho, Rais Magufuli amesema, serikali yake imekuwa ikijitahidi kurejesha utawala wa sheria, kupiga vita rushwa, ufisadi pamoja na kurejesha uwajibikaji kwa watumishi wa umma na wananchi ili taifa liende mbele.

“Nikigeuka huku nasikia kuna barabara hewa, nikigeuka tena nakutana na vyuo vikuu hewa, wanafunzi hewa, mikopo hewa na bado kuna wafanyakazi hewa, mzee wangu Kikwete umeniachia kazi ngumu kwelikweli,” amesema Rais Magufuli.

 

error: Content is protected !!