Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli alia na CCM Kigoma
Habari za Siasa

Magufuli alia na CCM Kigoma

Spread the love

JOHN Pombe Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 amesema, kinachoimaliza chama hicho Mkoa wa Kigoma kiko ndani ya chama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 18 Septemba 2020 katika mkutano wake wa kampeni za urais uliofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Mgombea huyo, ametumia mkutano huo kueleza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ndani ya Jimbo la Kigoma Mjini ambalo lilikuwa likiongozwa na Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo.

Amesema, ilani ya uchaguzi iliyotekelezwa ilikuwa ni ya CCM “na wala asije mtu hapa akasema alifanya yeye” huyo mumuogope kwani huo ndiyo ukweli wenyewe.

Katika mkutano huo, Rais Magufuli amewanadi wagombea ubunge kutoka majimbo yote ya Kigoma akiwamo Shaban Kirumbe anayegombea Kigoma Mjini.

Kirumbe anachuana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Zitto anayetetea nafasi hiyo.

Rais Magufuli amesema, wanachama wa CCM Kigoma vigeugeu na kwa sababu ikifika mchana wanakuwa CCM na usiku wanakuwa chama kingine.

“Tatizo la Kigoma liko ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa sababu mchana mnakuwa CCM, usiku mnakuwa chama kingine,” amesema Rais Magufuli.

Amewaomba wananchi wa Kigoma wampe kura za kutosha katika uchaguzi pamoja na kuwachagua wagombea wa CCM, ili chama hicho kifanikiwe kuunda Serikali huku akiahidi kuleta mabadiliko mkoani humo.

“Maendeleo hayana chama, tunataka Kigoma tuibadilishe, kwa mipango yote niliyonayo kwa Chadema hii miaka mitano itakuwa ya mwisho nataka mniletee wabunge wa CCM.

“Mimi najua namna ya kuwadhibiti, Kigoma tuna matatizo gani? hebu tufanye mabadiliko mwaka huu na mimi mnifurahishe kweli kweli,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewaeleza wananchi wa Kigoma kwamba, anaupenda sana mkoa huo kiasi cha kumpelekea kuteua mawaziri watatu kutoka katika mkoa huo.

Mawaziri hao ni, Dk. Phillip Mpango (Fedha na Mipango), Prof. Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi na Teknolojia) na Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri Uchukuzi na Mawasiliano.

“Nilipoteuliwa nilisema lazima nipange mikakati ya kutosha kupata mawaziri wa kutosha kutoka Kigoma, nikasema lazima niwe na waziri wa fedha anayesimamia Tanzania nzima, lakini lazima atoke Kigoma, nawapa hii siri wana Kigoma wanaotaka kuamini waamini wasioamini Mungu yupo,” amesema Dk. Magufuli.

Rais Magufuli amesema “Nikawa na mawaziri watatu angalieni ni mkoa upi Tanzania una mawaziri watatu? Tena mawaziri walioshika maeneo muhimu, nilifanya hivyo ndugu zangu kwa makusudi na niliamua nilaumiwe lakini nitoe upendeleo wa dhati Kigoma.”

Amesema aliamua kufanya hivyo ili asitokee mtu wa kumkwamisha maendeleo ya mkoa wa Kigoma.

“Nialifanya hivyo kwa sababu moja, ikitokea miradi Kigoma asitokee wa kuikwamisha, ili niinue Kigoma, nikamchagua Ndalichako yeye ni msomi mzuri, naye nikampa ubunge na uwaziri wa elimu na baadae nikamchukua Nditiye nikampeleka wizara ya ujenzi,” amesema Dk. Magufuli.

Ameahidi neema wananchi wa Kigoma endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania akisema kwamba, atanunua meli mbili (ya mizigo na abiria) pamoja na kurabati meli ya Mv. Sangara pamoja na kujenga bandari kubwa na ya kisasa.

“Nayaeleza haya Kigoma leo tarehe 18 mwaka 2020 andikeni kwenye kumbukumbu yenu kwamba ninayosema yanatoka moyoni tumepanga kununua meli kubwa ambazo zitafaya kazi Ziwa Tanganyika mimi sitoi ahadi hewa, meli moja itabeba watu 600 pamoja na tani 400, na ya pili itabeba mizigo tu tani 4,000,” ameahidi Rais Magufuli.

“Tunataka mwelekeo mpya wa kutengeneza Kigoma mpya kujenga bandari na jengo la abiria na ghala la kuhifadhi mizigo, tunataka Bandari ya Kigoma iwe ofisi kuu ya kuhudiamia bandari zote za ukanda wa ziwa Tanganyika,” ameahidi Dk. Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!