January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli akumbushwa kuleta Katiba Mpya

Spread the love

ASASI mbalimbali za kiraia (AZAKI) zimemtaka Rais Mteule, John Magufuli kuhakikisha analeta Katiba Mpya ili kubadirisha maendeleo ya nchi na kuondoa matatizo mbalimbali yanayotokana na mfumo mbovu wa katiba ya sasa. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Asasi hizo zinazojihusisha na masuala mbalimbali ya kisheria, kijamii, kisiasa na utamaduni zimesema hayo katika mjadala uliofanyika katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, uliozungumzia mambo ambayo Asasi za kiraia zinategemea kuyaona katika uongozi wa serikali mpya.

Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa amesema serikali mpya ni vyema ikaheshimu haki za binadamu ambazo ni nguzo kubwa katika utawala wa sheria.

“Tunahitaji kuiona Tanzania ikiheshimu haki za binadamu na amri za kikatiba hivyo katiba mpya ndio itakayosimamia misingi yote hiyo katika usawa,” anasema Olengurumwa.

Olengurumwa ambaye ndiye mwanzilishi wa mjadala huo amesema mambo mengine ambayo Asasi za kiraia inatarajia kuona ni mgawanyo mzuri wa kazi kwa viongozi ili kuongeza ufanisi kwa kila uongozi ufanye kazi katika kitengo husika.

Kuwepo kwa kasi ya uwazi na kasi ya uwajibikaji wa serikali Olengurumwa analizungumzia kuwa ni jambo linalowaumiza sana wananchi kutokana na rushwa zinazopitiliza kwa viongozi wasio wawajibikaji.

Ilani hizo za asasi za kiraia zenye ujumla wa ilani nane ambazo nyengine ni pamoja na, usawa wa kijinsia, usimamizi wa maendeleo, kukubalika na kushirikishwa kwa asasi za kiraia pamoja na upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

Olengurumwa amesema asasi za kiraia ni wadau muhimu sana katika maendeleo ya nchi yeyote wakiwa wanafanyakazi kwa maslahi ya umma na kusema kuwa tunaitaka serikali mpya iangalie asasi hizi na itambue kuwa zinamchangi mkubwa katika maendeleo.

error: Content is protected !!