Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli akumbusha machungu ya Waziri Mkuu Pinda
Habari za Siasa

Magufuli akumbusha machungu ya Waziri Mkuu Pinda

Hayati John Magufuli
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amekumbusha ‘machungu’ ya Mizengo Pinda, aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya awamu ya nne kuhusu bomoabomoa ya Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amekumbushia mvutano huo akisema, alipokuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, alitaka kuvunja sehemu ya jengo hilo iliyojengwa katika hifadhi ya barabara, ili kupisha ujenzi wa barabara lakini Waziri Mkuu, Pinda alimpinga.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Daraja la Juu la Kijazi, Ubungo Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 24 Februari 2021.

Amesema, baada ya kuingia madarakani, aliamua kufuata sheria kwa kulivunja jengo hilo, kisha kuanza ujenzi wa barabara ikiwemo daraja hilo.

“Namkumbuka mtani wangu Pinda akiwa waziri mkuu wakati huo, akaniambia kweli mtu anaweza akaenda kuvunja jengo la Tanesco? Sasa mwambie Pinda jengo la Tanesco tumelivunja, tuko hapa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, alichukua hatua hiyo ili kukidhi matakwa ya sheria dhidi ya watu waliokiuka sheria kwa kujenga ndani ya hifadhi ya barabara.

“Mtanishangaa huyu anamsema aliyekuwa waziri mkuu wake, ndio sababu sheria ni msumeno, nawaomba watendaji wasimamie sheria.”

“Haiwezekani ukaenda kubomolesha watu Kimara, ukawaacha waliovunja sheria, wengine walio ndani ya serikali, tutakuwa tunawaonea wananchi,” amesema Rais Magufuli.

Mizengo Pinda

Mbali na kukumbushia ‘mvutano’ wake na Pinda, amesema, kuna baadhi ya watu ndani ya serikali walimshangaa kufuatia hatua yake ya kubomoa yaliyokuwa majengo ya Ofisi ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam.

“Hapa tulipokaa, ilikuwa ndiyo Makao Makuu ya Tanroad Dar es Salaam, kama yupo hapa Mhandisi Ndiyamkama ilikuwa ofisi yake nikaja nikabomoa, walinishangaa kweli hata ndani ya serikali walinishangaa,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, hatua yake imefanikisha ujenzi wa barabara na daraja hilo “lakini ni kweli, sisi serikali hatuwezi kuongoza kwenye kuvunja sheria, sheria ni msumeno. Leo pamependeza, jengo hili nilisema hiki kipande cha Tanesco kiko ndani ya barabara.

1 Comment

  • Big up our president.Njoo kasulu vijijini uone kero za migogoro ya ardhi.wananchi tunateseka huku. thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!