July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli akumbana na nguvu ya Ukawa Mwanza

Spread the love

MGOMBEA wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana alikumbana na nguvu ya Ukawa, wakati akisalimiana na wakazi wa kata ya Mabatini jijini hapa. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Magufuli ambaye yupo mkoani Mwanza, akiendelea na kampeni zake, alikumbana na kasheshe hilo eneo la Mabatini, Nyamagana wakati akielekea wilayani Magu, saa 2:30 asubuhi.

Magufuli akiwa katika eneo la Mabatini wakati akiwapungia wananchi mkono, baadhi ya vijana waliohudhulia walionekana wakionesha ishara ya vidole viwili huku wakishangilia kwa kuimba people peoples.

Hata hivyo wakati vijana hao waendelea kuimba Peoples peoples huku wakilitaja jina la Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, anayeungwa mkono na kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakidai kwamba ndiye Rais wa awamu ya tano.

Pia wakati vijana hao wakiendelea kuimba huku wakilitaja jina la Lowassa kuliibuka vurugu kati ya vijana wanaotajwa kuwa wa Chadema na CCM ambako vurugu hizo zilizimwa na walinzi wa Magufuli.

Hata hivyo hali iliyosababishwa na mfuasi mmoja wa Chadema aliyepita akiwa kwenye pikipiki iliyofungwa bendera, hali iliyoibua kelele wakati wananchi waliokuwa barabara wakimsubili Magufuli apite.

Mmoja wa wananchi wa Kata ya Mabatini, Samwel Lissu, amesema wakati wakimsubili mgombea huyo alitokea kijana mmoja ambaye hakufahamika jina lake aliyepita akiwa na bendera ya Chadema na kuibua kelele.

“Hapa watu waliokuwepo wana itikadi tofauti, kwa sababu leo ni wikiendi watu walipotangaziwa kwamba Magufuli anapita hapa, walikusanyika, kamanda mwenzetu alipopita lazima tushangilie,” amesema Lissu.

Hata hivyo Magufuli ambaye juzi alikuwa na mkutano katika uwanja wa Furahisha, ambako umati wa watu uliojitokeza walikuwamo wanafunzi wa shule za sekondari za Ngaza na Nsumba ambao inadaiwa walilazimishwa kuvaa nguo za kiraia.

Hata hivyo baada ya mkutano huo kumalizika, wanafunzi hao walitelekezwa uwanjani hapo, mpaka saa 3:00 usiku kufuatwa na gari za kusombea uchafu na kupelekwa katika maeneo ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana ambako inadaiwa walilala katika ukumbi wa mikutano wa Grand.

Inadaiwa kuwa agizo la wanafunzi hao kwenda kwenye mkutano, lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ambaye alituma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi, kwenda kwa walimu wa shule mbalimbali za mkoa huo.

Mwanahalisi Online, ilishuhudia magari mbalimbali ikiwasomba watu kutoka maeneo tofauti ya kanda ya ziwa, ikiwemo Mara, Geita na Simiyu na viunga vyake ili kujaza uwanja huo ambao hata hivyo haukujaa kama uliyofanywa na Ukawa Oktoba 12 Mwaka huu.

Mulongo alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo yake ya mkononi haikupatikana.

error: Content is protected !!