July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli akikosea kwa Waziri Mkuu, amechemsha

Spread the love

BAADHI ya viongozi wa dini na jamii kwa ujumla wamemtaka Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli kuhakikisha anampata Waziri Mkuu mchapa kazi na si vinginevyo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Waliyasema hayo kwa vile wanaamini Waziri Mkuu ndiyo msimamizi mkuu wa mambo yote ya serikali, hivyo kukosea kwake kunaweza kukamfanya akashindwa kutekeleza ahadi zake.

Askofu wa Kanisa la Methodist jimbo la Dodoma, Joseph Bundara, amesema ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima apatikane waziri mkuu mwenye kusimamia maamuzi yasiyotetereka.

“Kwa sasa taifa letu wananchi wake wana hali mbaya kiuchumi hivyo wanakabiliwa na umasikini wa kutupwa huku kundi la watu wadchache wakijineemesha.

“Ili kuondoa hilo waziri mkuu ambaye ni msimamizi mkuu wa serikali anatakiwa kuhakikisha anasimamia misingi ya utawara bora ikiwa ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumiwa vizuri na kuwanufaisha wananchi wote,” amesema Askofu Bundara.

Mbali na hilo alimtaka Rais Dk. Magufuli kuhakikisha anasitisha matumizi mabaya ya rasilimali za serikali ambayo kwa hatua kubwa yamesababisha nchi kuyumba na kuwafanya watanzania kuwa masikini.

Naye Hawa Makau, ambaye ni mkazi wilayani Mpwapwa, amesema ili taifa liweze kusonga mbele ni lazima baraza la mawaziri liwe dogo na lenye tija.

Aidha amesema rais huyo wa awamu ya tano anatakiwa kuwachagua mawaziri na manaibu ambao ni wachapa kazi na asiangalie ukanda wala kutoa nafasi hizo kwa upendeleo.

“Taifa hili lina watu wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi lakini mara nyingi hawapewi nafasi hizo kwa sababu ya viongozi wa juu kulindana na kubebabana na wakati nafasi hizo upeana watoto wa wakubwa.

“Nafasi za uongozi zitolewe kwa kuzingia ujuzi na uelewa wa mtu na isiwe fadhila au kutomteua mtu mwenye uwezo kwa sasabu binafsi za chuki,” alieleza Makua.

Licha ya uteuzi wa Mawaziri na Manaibu wake pia Makau alizungumzia kuhusu suala la uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa kuwa nao ulenge kwa vijana ambao wametoka vyuoni wenye taaluma badala ya kuendelea na waliopo kwa sasa ambao hata wao wanaonekana kushindwa kazi.

“Mimi najiuliza maswali mengi ni kwanini wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wanachaguliwa hao hao tu wakati wapo vijana wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo,” alieleza mwananchi huyo.

error: Content is protected !!