August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli aanza kusafishwa

Spread the love

AMOS Siyantemi, Mwenyekiti wa kampeni ya vitabu na mdahalo (KVM) amesema Dk. John Magufuli, rais wa Tanzania si dikteta kama watu wanavyosema, anaandika Hamisi Mguta.

Siyantemi ameyasema hayo wakati akizundua kitabu chake cha ‘majipu ya nchi yetu tushirikiane kuyatumbua’ ambacho ameeleza kuwa kina maudhui ya kuchochea moyo wa kizalendo, uwajibikaji kwa viongozi na wananchi.

Pamoja na rais Magufuli, kufuatia mtiririko wake wa matukio mbalimbali ya utumbuaji wa majipu chini ya sera yake ya ‘Hapa Kazi tu’ ambayo inalalamikiwa na wengi kuwa haitendi haki na inanyima uhuru wa kijieleza, Siyantemi amesema wanaompinga ni wanafiki.

“Tuwe makini na baadhi ya wanasiasa  wanaotaka kuwa maarufu kisiasa, raisi wetu si dikteta kama watu wanavyosema,..ni wanasiasa wanafiki, malimbukeni, wamefirisika sera wanamchafua rais kwa kugeuza kauri,” amesema.

Ameeleza kumekua na kauri mbalimbali zinazoonesha uchochezi hali ambayo itasababisha kutoelewana wenyewe kwa wenyewe.

Ameongeza kuwa kauli ya wanasiasa kusema ‘hawatambui uchaguzi wa marudio Zanzibar’ ni yakichochezi hivyo wanasiasa waangalie kauli za kuongea kwani nchi itakwenda pabaya.

Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amesifu kitabu kicho na kusema kuwa kinaelezea majipu yaliyopo nchini, kutolea ufafanuzi wa tabia ya ulafi wa mali na watumishi hewa.

Amesema kitabu hicho kinaenda sambamba na sera za chama cha mapinduzi na kuwa kiloa anachokifanya rais si rahisi pekee bali ni sera za chama.

“Kuna watu hadi sasa wanaamini kwamba kila kinachofanywa na rais lakini vipo ndani ya sera za chama,” amesema.

 

error: Content is protected !!