Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Magori asimulia siri ya Hans Pope kumpindua Mwalimu Nyerere
MichezoTangulizi

Magori asimulia siri ya Hans Pope kumpindua Mwalimu Nyerere

Crescentius Magori, mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Simba
Spread the love

 

CRESCENTIUS Magori, mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Mohamed Dewji amesema, kifo cha Zacharia Hans Pope (64) ni pigo kubwa ndani ya timu hiyo. Anaripoti Damas Ndelema, TURDACo … (endelea).

Hans Pope alifikwa na mauti tarehe 11 Septemba 2021, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake, umeagwa leo Jumatatu, 13 Septemba 2021, katika viwanja vya Karimjee, jijini humo.

Mwili wa Hans Pope aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Simba na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa mabingwa hao mara nne mfululizo wa Tanzania Bara, utazikwa keshokutwa Jumatano tarehe 15 Septemba 2021, kijijini kwao Kihesa Mkimbizi, Mkoa wa Iringa.

Magori ametumia dakika zisizozidi 15 kuelezea jinsi walivyoshia na Hans Pope ndani na nje ya timu hiyo huku akidokeza jinsi alivyomuuliza mkasa wa Hans Pope, akiwa Luteni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wenzake kutaka kumpindua Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo Hans Pope akiwa na miaka 28.

“Kuna siku tukiwa kwenye stori, nikamuuliza ulifikiria nini ukiwa na miaka 28 tu kutaka kupindua na kumpindua mtu mwenyewe ni Mwalimu Nyerere? Akasema anatamani sana kuandika kitabu lakini wenzangu tuliokuwa nao hawataki waandikwe lakini hao watu wanaokataa kama wakifariki kabla yake basi ataandika kitabu lakini Mungu amemchukua kabla hajaandika,” amesema Magori

Fuatilia zaidi simulizi ya Magori;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!