January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magari 1,400 yanaswa kwenye oparesheni

Kamishna Diwani Athumani, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Spread the love

JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbalimbali za kiserikali katika oparesheni usalama 11, limekamata magari 1,400 yaliyoingizwa nchini bila kibali maalumu.Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Katika oparesheni hiyo pia, wamekamata watuhumiwa 141 wa makosa mbalimbali ya jinai, wakiwemo wahamiaji haramu, silaha haramu, dawa za kulevya na nyara za serikali.

Akizungumzia oparesheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, amesema ilichukua siku mbili kati ya Juni 4-5 mwaka huu.

Athmani amesema, oparesheni hiyo pia ilihusisha ofisi za Polisi wa Kimataifa (Interpol) Kanda ya Kusini mwa Afrika, ambapo maamuzi ya zoezi hilo yalitokana na mkutano mkuu wa wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika na Mashariki.

“Katika mkutano huo, tulikubaliana kufanya opareshani ya pamoja na siku moja ambapo tulishughulika na makosa ya wizi, madawa ya kulevya, silaha haramu, ugaidi, biashara haramu na makosa mengine,”amesema Athuman.

Kwa upande wa Tanzania, mikoa iligawanywa katika kanda nane, ambazo ni, Kanda ya Kusini, Dar, Ziwa, Kati, Zanzibar na nyingine, ambapo tuliwabaini watuhumiwa hao.

Athuman ameongeza kuwa, licha ya kuwakamata watuhumiwa hao, bado wanaendelea na uchunguzi zaidi na kwamba, oparesheni hiyo ilitakuwa endelevu nchini.

Ameagiza wananchi wote wanaomiliki silaha bila kibali maalum, wajitokeze na kuzisalimisha katika kituo cha polisi chochote kabla ya msoko kupita.

“Natoa ofa, kwa yeyeto yule atakayeleta silaha yake yenye makosa kwetu ndani ya miezi hii mitatu, hatachukuliwa hatua yoyote ya kisheria maana atakuwa ametii sheria bila shuruti,”amesema Athuman.

error: Content is protected !!