December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Maganda ya korosho yana thamani  kubwa kuliko korosho yenyewe’

Geofrey Mwambe, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

Spread the love
GEOFREY Mwambe, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amesema, zao la korosho lina thamani kubwa lakini bei ya zinazoliwa ni asilimia 5 au 10 ya thamani yote. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mwambe amesema, hivi karibuni wamefanya kongamano lililokutanisha wawekezaji mbalimbali mkoani Mtwara, ambapo wawekezaji kutoka nchi mbalimbali walioshiriki wamewafungua macho juu ya zao hilo kuwa na thamani kubwa kuliko inavyodhaniwa.

Amesema, ukubwa wa thamani ya zao hilo ni kutokana na kuuzwa kuanzia tunda (bibo), maganda hadi korosho yenyewe na kuwa, thamani ya bibo au maganda ni kubwa kuliko korosho yenyewe.

“Yale matunda ya korosho unatengenezea juisi, Wine ambazo zinauzwa kwa gharama kubwa, lakini pia unaweza kutengeneza hata pombe kali au biskuti.

“… hivyo wawekezaji wametufungua macho kwasababu kuna wengine wanataka maganda tu kwa ajili ya kukamua mafuta, wametuonyesha ni jinsi gani maganda yana thamani kuliko hata korosho yenyewe,” amesema.

Mwambe amesema, korosho zinazoliwa pia zinaweza kutumika kutengeneza ‘maziwa ya korosho’ ambayo pia yanaweza kuuzwa na kuliongezea thamani zao hilo hivyo kipindi cha nyuma  nchi ilikuwa hainufaiki na zao hilo.

“Korosho pia zinatumika kutengeneza maziwa kama yale ya Soya na kupakiwa kwenye maboksi ni kitu ambacho hakikuwahi kufikirika kama zao la Korosho linaweza kuleta kitu cha namna hiyo,”amesema.

error: Content is protected !!