June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magaidi 30 wauawa Msumbiji

Spread the love

 

WANAJESHI wa Rwanda, walioko nchini Msumbiji kukabiliana na ugaidi, wamewauwa wanamgambo wa kiislamu 30, waliovamia Jimbo la Cabo Delgado, Kaskazini mwa nchi hiyo. Inaripoti BBC … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na mamlaka za usalama nchini Msumbiji.

Mamlama hizo zimesema kuwa, wanamgambo hao wa kiislamu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Al Shabab, waliuawa katika doria zilizofanywa na Wanajeshi wa Rwanda, katika msitu ulioko karibu na mji wa bandari ya Palma.

Serikali ya Rwanda mwanzoni mwa mwezi huu, ilituma wanajeshi wake 1,000 kwa ajili ya kukabiliana na magaidi hao, wanaoisumbua Msumbiji zaidi ya miaka minne.

Pia, nchi ya Ureno na Jumuiya za Kusini mwa Afrika, zimepeleka wanajeshi kwa ajili ya kukabiliana na wanamgambo hao. Ikiwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji.

Wanamgambo hao wamewauwa maelfu ya watu, huku watu zaidi ya laki nane, wakikimbia makazi yao.

error: Content is protected !!