July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Mafunzo ya vitendo yameongezwa’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Spread the love

SERIKALI imesema, kwa sasa wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo zaidi ili waweze kuelewa lugha katika kile wanachojifunza. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe, Prof. Kulikoyela Kahigi (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuwafanya kuwa na uelewa wa lugha kwa wanafunzi ambao wanafundishwa tofauti na ilivyo kwa sasa.

“Uelewa mdogo wa wanafunzi unatokana na njia mbovu ya ufundishaji. Je, serikali itatumia njia gani ya kutatua tatizo hilo,” alihoji Prof. Kahigi.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) alitaka kujua ni lini Sera ya Elimu iliyoidhinishwa na Rais Jakaya Kikwete itakuwa mkombozi wa elimu?

Nyangwine alitaka kujua serikali imefanya mapinduzi yapi ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia viwango vyote vya elimu kwa mujibu wa sera hiyo.

Katika swali hilo mbunge alitaka kujua matumizi ya kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo katika Elimu ya Msingi kwa mujibu wa sera hiyo siyo tishio kwa waandishi na wachapishaji wa vitabu na serikali inashauri nini kwa wadau hao.

Akijibu swali la nyongeza la Prof Kahigi, Majaliwa alisema kuwa, kwa sasa wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo zaidi ili kuweza kutambua kwa lugha wanayojifunzia.

Kwa upande wa majibu ya swali la msingi Naibu Waziri  Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango amesema, matumizi ya kitabu kimoja cha kiada yataondoa mkanganyiko katika Sekta ya Elimu uliotokana na tofauti za upimaji wa ufundishaji na ujifunzaji na kusababisha wanafunzi wengi kushindwa mituhani.

Alisema, wanafunzi wengi wameonekana hawajui kusoma na kuandika jambo ambalo ni hatari kwa elimu ya kitanzania.

error: Content is protected !!