Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mafunzo ya kujitolea JKT 2020/21 yasitishwa
Habari Mchanganyiko

Mafunzo ya kujitolea JKT 2020/21 yasitishwa

Spread the love

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) nchini Tanzania, limesitisha mafunzo ya JKT kundi la kujitolea kwa mwaka 2020-2021. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kutokana na usitishwaji wa mafunzo hayo, limewataka vijana ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena na wale ambao wamefika warejee nyumbani.

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 19 Januari 2021 na Kaimu Mkuu wa Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kanali Mabena amesema, mafunzo hayo yalikuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini hivyo wameyasitisha kwa muda mpaka hapo itakapotangazwa.

Amesema kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT ya kujitolea warejee majumbani kwao.

Kanali Mabena amesema na wale ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!