June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mafunzo TaGLA yanufaisha 20,322

Spread the love

WAKALA wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Tanzania (TaGLA) wameendesha mafunzo kwa washiriki 20,322 ambapo jumla ya midahalo 783 imefanyika kuanzia 2005 mpaka Juni 2015. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Taasisi hiyo pia imekutoa mafunzo kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wawaziri, wakuu wa taasisi za umma na binafsi ambapo wamekuwa wakishirikiana na taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Charles Senkondo amesema kuwa walianzisha mtandao huo ili kuongeza uwezo wa kufanya kazi na ubunifu zaidi kwa njia za kisasa.

Akielezea kazi zinazofanywa na TaGLA amesema ni kutoa nafasi kwa mataifa ya nje kutoa elimu nchini, kuwezesha ukuaji wa taaluma kupitia mitandao mbalimbali duniani, kuwezesha wadau kujifunza kwa kutumia mazingira mazuri yenye gharama nafuu.

Kazi nyingine ni kuendelea kuwa jukwaa la mafunzo na midahalo, kutekeleza jukumu la kukuza sera za serikali, kukuza matumizi ya teknolojia katika nyanja mbalimbali za maendeleo nchini.

Nyingine ni kutoa mafunzo yanayowezesha Watanzania kwenda na teknolojia kwa ajili ya kuzoboresha huduma, kutoa ushauri katika maeneo mbalimbali ya kiufundi na kitaalamu.

Awali, TaGLA ilianzishwa kuchukua majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo ya Dunia Tanzania (TGDLC) kupitia toleo la Na 445 la gazeti la serikali lililochapishwa Desemba 23, 2011 ambapo Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue aliizindua rasmi Julai 12 mwaka 2012.

error: Content is protected !!