
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, amesema zoezi la uwekezaji anuani za makazi limefikia asilimia 95 na kwamba maeneo yote ya Tanzania kwa sasa yanapatikana kwenye mtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).
Simbachawene amesema hayo leo Ijumaa, tarehe 1 Julai 2022, akizungumza katika halfa ya kufunga mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, iliyofanyika mkoani Iringa.
Amesema, kwa sasa zoezi lililobaki ni uwekaji anuani hizo katika miundombinu ikiwemo uwekaji vibao vya majina ya mtaa kila eneo.
“Operesheni ya anuani na makazi imefikia asilimia 95, hii ikiwa ni muunganiko wa utekelezaji wa shughuli zote zilizopangwa. Kazi zinazoendelea kufanyika sasa kuweka miundombinu za anuani za makazi zinazounganisha nguzo na majina ya barabara na kubandika vibao vya namba za nyumba,” amesema Simbachawene na kuongeza:
“Kidigitali nchi yetu sasa ina majina, mitaa, kila eneo limewekwa sawa isipokuwa kidigitali takwimu wanaisafisha kuweka sawa. Kimiundo bado asilimia tano ili tuweze kuweka kibao kila mahala.”
More Stories
Dk. Mpango atoa somo Wimbo wa Taifa
Basilla ataka kero za wananchi zotatuliwe
Samia aungana na viongozi Afrika kumpongeza Ruto