December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maeneo yaliyotwaliwa na JWTZ yameanza kulipwa – Waziri Mwinyi

Spread the love

MBUNGE wa Mtambile, Masoud Salim (CUF) ameihoji Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lini italipa fidia wananchi waliotwaliwa maeneo yao na Jeshi la Wananchi (JWTZ). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 15 Mei 2019, Salim amehoji kwa nini serikali imejikita katika utekeleza ji wa ujenzi wa miradi mikubwa na kusahau kulipa stahiki za wananchi.

Salim amesema, kitendo cha serikali kuchelewa kulipa fidia wananchi, kinaweza sababisha baadhi ya wananchi kutopata haki zao kwa kuwa  baadhi yao wamefariki dunia pasipo kulipwa.

“Imekuwa ni muda mrefu baadhi ya ameneo wananchi wamfariki dunia pasipo kulipwa fidia, na serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa kwa fedha za ndani, kwa nini mmechukua muda mrefu kulipa wananchi ilihali mnatekeleza miradi mikuwa kwa fedha za ndani,” amehoji Salim.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi amesema si kweli kwamba serikali imekawia kulipa fidia wananchi, kwa kuwa imekwishaanza kulipa fedha baadhi yao.

Dk. Mwinyi amesema hadi sasa takribani Sh. 3 bilioni kati ya 20.9 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya kulipa wananchi fidia  zimetolewa na serikali, na kwamba kiasi kilichobakia kitalipwa kwa wahusika baada ya kufanyiwa uhakiki.

“Kweli yako maeneo yalichukuliwa na Jeshi,  baadhi yalilipwa fidia na mengine mchakato wa kulipa fidia wananchi unaendelea, mpango wa serikali ni kulipa fidia wananchi kwa kadri ya uwezo wake. Sh.  20.9 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia,” amesema Dk. Mwinyi na kuongeza,

“Uhakiki wa madeni ya fidia unaendelea kama kawaida, nawaomba wananchi wawe na subira wakati serikali inafanya uhakiki kwa ajili ya kulipa fidia zao.”

error: Content is protected !!