Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Maelfu waaga mwili wa Floyd
Kimataifa

Maelfu waaga mwili wa Floyd

Spread the love

MAELFU ya Wamarekani, wamejitokeza katika Kanisa la Houston kuuaga mwili wa George Floyd, mmarekani mweusi aliyeuawa na polisi wa Minnesota na kusababisha kuibuka kwa maandamano ndani na nje ya taifa hilo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Waombolezaji hao waliovaa fulana zenye picha ya Floyd, wametoa heshima zao za mwisho leo tarehe 9 Juni 2020, kabla ya mwili huo kuzikwa jijini humo. Watu zaidi ya 6,000 wanatajwa kuhudhuria mazishi hao.

Kifo cha Floyd kimechukuliwa kwa uzito wa pekee baada ya Wamarekani kuchoshwa na mauaji ya watu weusi, vifo vingine vinavyotajwa kabla ya Floyd ni cha Eric Garner, Michael Brown, Ahmaud Arbery na Trayvon Martin.

Kwenye salamu hizo za mwisho, Philonise Floyd ambaye ni kaka wa Floyd amesema “inaumiza sana,” kushiriki mashizi yaliyosababishwa na walinda usalama wa raia na mali zao.

Jeneza la Floyd limesindikizwa na polisi wa Houston mpaka kanisani ambapo taratibu zote zimesimamiwa na polisi hao, kwa utaratibu unaokubwalika.

Awali, akizungumza na wakazi wa Texas, Philonise amesema kinachofanyika Marekani kwa sasa ni kikubwa kuliko mdogo wake George kwa kuwa, kinakwenda kubadilisha kila kitu.

“Hiki kinachofanyika ni kikubwa kuliko George kwa sasa. Tumefanikiwa kuzuia hofu za raia kwa polisi,” amesema Philonise.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!