Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Maelfu Myanmar walivimbia jeshi
Kimataifa

Maelfu Myanmar walivimbia jeshi

Spread the love

 

MAELFU ya wananchi wa Myanmar wamejitokeza katika miji mbalimbali nchini humo, wakipinga utawala wa kijeshi. Inaripoti Aljazeera…(endelea).

Taarifa kutoka Myanmar zinaeleza, kwamba biashara zilifungwa sambamba na baadhi ya huduma za kijamii katika sehemu kubwa ya nchi hiyo, huku idadi kubwa ya watu ikijitokeza kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa tarehe 1 Februari 2021.

Licha ya jeshi la nchi hiyo kuonya, kwamba vifo vingi vitatokea iwapo waandamanaji wataendelea kujitokeza, idadi ya watu Jumapili wiki iliyopita imerekodiwa kuwa kubwa zaidi ya siku zote tangu maandamano hayo kuanza.

Tarehe 1 Februari 2021, Jeshi la Myanmar lilitangaza kudhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini humo.

Ni kutokana na siku kadhaa za mvutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi. Jeshi hilo limedai kufanya kutokana na kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka 2020.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD), kiliongoza ambapo Aung San Suu Kyi aliibuka mshindi.

Kutokana na maandamano hayo, Marekani imelieleza jeshi la Mnyamar, kwamba inaweza kuchukua hatua iwapo haki za raia wa nchi zitakandamizwa katika kipindi hiki cha maandamano.

Imeelezwa, madai ya waandamanaji wa Myanmar ni kutaka uchaguzi wa haraka ili nchi hiyo itoke kwenye mikono ya jeshi ambalo linaelezwa kuendesha vitendo vya kikatili dhidi ya raia wa taifa hilo.

Idadi kubwa ya waandamanaji imeshuhudiwa katika Mji Mkuu wa Taifa hilo, Yangon wakitaka hatua ya kwanza jeshi hilo kuwaachia bila masharti viongozi wote waliowakamata kabla na baada ya mapinduzi.

Licha ya jua kali pia vitisho kutoka kwa jeshi la nchi hiyo, watu wamejitokeza kupaza sauti zao huku mji wa pili kwa ukubwa Naypyidaw, uksishuhudia shule na huduma za vyakula zikifungwa. Hali hiyo imejitokeza kwenye miji ya Myitkyina, Hpaan, Pyinmana,Dawei na Bhamo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!