WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanania, imetenga fedha kwa ajili ya kujenga maegesho ya Kayenzi na Kanyinya. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 18 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ngara (CCM), mkoani Kagera, Ndaisaba Ruhoro.
“Je, ni lini serikali itapeleka Kivuko Mto Ruvuvu ili kuunganisha vijiji vya Mayenzi na Kanyinya vilivyoko wilaya ya Ngara,”ameuliza Ruhoro
Waitara amejibu, serikali imepanga kuendeleza kuboresha huduma za usafiri kwa njia ya maji, ikiwa ni pamoja na kuunganisha maeneo yenye mahitaji ya vivuko ikiwemo Kayenzi na Kanyinya kila inapopata fedha.
Amesema, aidha katika mwaka wa fedha 2021/22, serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maegesho hayo.

“Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania(Temesa)uko kwenye hatua za ununuzi wa kumpata mkandarasi wa kufanya ujenzi wa maegesho ya kivuko
hicho.”
“Mkandarasi wa kufanya ukarabati wa kivuko kidogo, chenye uwezo wa kubeba abiria 60 na magari mawili ambacho hapo awali kilikuwa kinafanya kazi eneo la Rusomo-Nyakiziba(MV Ruvuvu ya zamani),”amesema Waitara.
Waitara amesema, baada ya ukarabati hupo kukamilika, kitatoa huduma kwenye eneo la kati ya Kayenzi hadi Kanyinya.
Leave a comment