August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maduka 150 yateketea Karagwe

Spread the love

MADUKA 150 yameteketea kwa moto katika Mji wa Kayanga, Karagwe mkoani Kagera ambapo chanzo cha tukio hilo hakijafahamika, anaandika Wolfram Mwalongo.

Moto huo umeanza kuteketeza maduka hayo jana saa mbili usiku kwenye Soko la Kayanga wilayani humo.

Hata hivyo, magari ya zima moto yamechelewa kufika kwenye eneo la tukio na kusababisha kiasi kikubwa cha mali kuteketea.

Kitendo cha magari ya zima moto kuchelewa kimewakera wafanyabiashara wa soko hilo ambao wamedai kuwa, kila mwezi hutozwa Sh. 30,000 ili kuchangia huduma ya zima moto wilayani hapo.

Magari hayo hulazimika kutoka katika Uwanja wa Ndege Bukoba mjini mpaka Karagwe mjini ikiwa ni umbali wa kilomita 120.

Akizungumza na waandishi wa habari jana usiku katika eneo la tukio Deodatus Kinwiro, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe amesema kuwa, serikali ya wilaya yake itapata gari la zima moto hivi karibuni.

“Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto, ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”

error: Content is protected !!