May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madrid, Liverpool vitani leo

Spread the love

 

HATUA ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA0 inataendelea hii leo, ambapo Real Madrid itashuka dimbani kuikabili Liverpool kwenye Uwanja wa Alfredo Di Stefano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)..

Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza utapigwa majira ya saa 4 usiku.

Liverpool imepoteza michezo mitatu ya nyuma dhidi ya Real Madrid walipokutana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.

Mara ya mwisho timu hizi zilikutana kwenye fainali ya michuano hiyo mwaka 2018 na Liverpool kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Katika mchezo wa leo Liverpool itaendelea kukosa huduma ya nahodha wake Virgil Van Djik ambaye alipata majeruhi ya muda mrefu.

Kwa upande wa Madrid wao watamkosa mlinzi wao wa kati raia wa Ufaransa, Raphael Varane ambaye amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mchezo mwengine leo utaikutanisha Manchester City ambao watakuwa nyumbani dhidi ya Borrusia Dortmund kutoka nchini Ujerumani na mchezo huu utachezwa majira ya saa 4 usiku kwenye Uwanja wa Etihad.

error: Content is protected !!