August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madiwani wataka walimu wabanwe

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

SERIKALI imeombwa kuweka kipengele kitakachowabana walimu ili wakubali kuishi vijijini na kwenye mazingira magumu, anaandika Christina Haule.

Na kwamba, uwekwe taratibu kwa wanaotaka kusomea fani ya ualimu kukubali mazingira yoyote ya kazi, vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Kauli hiyo imetolewa leo na madiwani wa kata tofauti mkoani Morogoro kwenye mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Victory Youth Support Organization (VIYOSO kwa ushirikiano na Foundation for Civil Society (FCS).

Ni baada ya kukutana na kujadili pia kuweka mikakati ya kuboresha elimu kwa kata zilizo pembezoni wilayani humo hususani Kata ya Kolero, Kasanga na Bungu.

Avelin Lucas, Diwani wa Kata ya Bungu na Boniface Banzi, Kata ya Kasanga wilayani Morogoro wametoa kauli hiyo na kwamba, ikiwa hatua hiyo haitachukuliwa, ifikapo mwaka 2018 vijiji nchini havitakuwa na wataalamu.

Amesisitiza kuwa, endapo serikali haitakuwa na sera sambamba na sheria itakayowalazimisha watumishi hao kuishi na kufanya kazi katika maeneo hayo, hali itakuwa ngumu zaidi.

“Ni kama serikali haina meno ya kuwalazimisha watumishi wa umma wakiwemo walimu kuishi vijijini bila kujali visingizio vya uongo kama ugonjwa, ndoa na vitisho vya kuacha kazi.

“Itungwe sera na sheria itayowamba na kuwalazimisha kuishi mazingira hayo,” amefafanua Lucas.

Madiwani hao wamesema endapo serikali itaweka moja ya kigezo cha kusomea fani fulani ni mwenye uwezo wa kuishi vijijini na mazingira magumu na atakayekiuka kushitakiwa, tatizo la wataalamu wakiwemo walimu vijijini litaisha.

“Mfano kata zetu hizi huku milimani shule yenye zaidi ya wanafunzi 700 ina kati ya walimu  wawili hadi watatu ambao pia ni wazee na  ni walimu wa kiume pekee wakati  katika kada hii pia wanahitajika walimu wa kike kwa malezo bora ya watoto wa kike,” amesema Lucas.

error: Content is protected !!