Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani wa CCM wamkataa Meya wao
Habari za SiasaTangulizi

Madiwani wa CCM wamkataa Meya wao

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire. Picha ndogo baraza la madiwani wa jiji hilo.
Spread the love

MADIWANI 19 kati ya 25 wa baraza la madiwani Jiji la Mwanza, wamesaini waraka wa kutokuwa na imani na Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire, wakimtuhumu kutumia vibaya mabaya yake, anaandika Moses Mseti.

Jiji la Mwanza linaongozwa na meya anayetokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) huku madiwani waliosaini waraka wa kutokuwa na imani na kiongozi huyo wanatokana na chama hicho tawala.

Madiwani hao wanamtuhumu Bwire, kwamba baada ya kuingia madarakani, alianza kupora viwanja vya halmashauri hiyo ikiwemo viwanja vilivyo kata ya Mahina anapojenga hospitali yake iliyo karibu na shule yake ya Alliance.

Tuhuma nyingine, ni kwamba amekuwa akifunga ofisi muda wowote anaoutaka na kwenda kufanya shughuli zake binafsi, kutumia gari la jiji kwenda kufanya shughuli zake na kushinikiza kuwekewa mafuta na kuisababishia halmashauri hasara.

Tuhuma nyingine zinazomkabiliwa Bwire ni zile za kumtuhumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba kwamba alifanya njama za kutaka kumwekea kitu kinahodhaniwa sumu ofisini kwake kitendo ambacho kimezorotesha utendaji kazi katika halmashauri hiyo.

Hoja hiyo ya kutokuwa na imani na Meya imeibuliwa leo dakika nne mara baada ya wimbo wa kuombea baraza la madiwani na ulipofika muda wa kuanza kwa bara hilo na Diwani wa Kata ya Mkolani Donatha Gapi, aliye nyoosha mkono na kuomba mwongozo.

Mara baada ya kuruhusiwa alisimama na kudai kwamba Meya Bwire tayari amepelekewa waraka wa madiwani wa kutokuwa na imani naye hana sifa za kuendelea kuongoza kikao hicho.

Diwani huyo amesema kuwa, meya huyo amekuwa akitumia vibaya madaraka yake, kitendo ambacho kimezorotesha utendaji kazi wa watumishi wa jiji, hivyo wamelazimika kuandika waraka na kuusaini ili wamng`oe katika kiti hicho.

Gapi amesema kuwa wanafahanya hivyo kuweza kupata mrejesho wa maazimio yao yalipofikia kwa kuwa tayari Meya huyo alishapewa nakala pamoja na mkurugenzi wa Jiji hilo Kiomoni Kibamba.

“Maazimio haya sio ya chama ni ya madiwani na tuliosaini waraka huu ni madiwani 19 kati ya 25, sisi tunataka kulinda maslahi ya wananchi haiwezekani mtu afanye ofisi kama taasisi yake binafsi,” amesema Gapi.

Diwani wa Mabatini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Deus Mbehe amesema kuwa Meya huyo alidiriki kufunga ofisi yake kwa kipindi cha miezi sita huku naibu meya, akifanyia shughuli nje ya ofisi.

“Madiwani tuliosaini ni wengi na wala sio wa CCM pekee hata baadhi yetu (upinzani) tumesaini huo waraka kwa muda mrefu meya amekuwa akitengeneza makundi ndani ya madiwani na kusababisha migogoro isiyokuwa na maana,” amesema Mbehe.

Mbehe amesema meya huyo anapaswa kuachia madaraka kwa kuwa tayari ameshindwa kufanya kazi za wananchi na kwamba pindi wanapojaribu kumshauri amekuwa akishindwa kusikiliza ushauri wao kwa madai wanamuonea wivu.

Meya huyo, amesema anawashangaa madiwani hao kuhoji vitu vya ajabu na kwamba wameshindwa kuhoji mambo ya msingi ikiwemo kikao kilichoazimia kuundwa kwa tume ya kuhusu dampo la Buhongwa lililojengwa kwa zaidi ya Sh. 600 milioni lakini lipo chini ya kiwango na vifaa vinavyotumika ni vya jiji kinyume na mkataba wa mkandarasi.

Amesema madiwani pia wangepaswa kuhoji ujenzi holela wa majengo unaofanywa katika jiji la Mwanza bila vibali na kwamba kikao kilichofanyika Machi mwaka huu kiliazimia tume kuundwa kuchunguza suala hilo lakini hakuna jambo lolote lililofanyika.

“Nilitengemea wahoji mradi wa maji wa Sh. 900 milioni ambao haufanyi kazi na kila siku pesa zinakusanywa zinaenda huko lakini hakuna na wananchi wa fumagila hawapati huduma ya maji safi na salama,” amesema Bwire

Bwire amesema yeye hajashindwa kufanya kazi na wala hajawahi kula rushwa huku akiwatuhumu madiwani wenzake kwamba wamekuwa wakidai kuwa amebana watumishi na wao (madiwani) wamekosa fedha zilizo nje ya posho na mshahara wao.

Amesema kuwa anaye wadanganya madiwani hao ni Mkurugenzi wa Jiji Kiomoni Kibamba kwamba, kukoswa kwao fedha kunatokana na yeye kubana watumishi hivyo wataondoka katika halmashauri hiyo wakiwa masikini.

Omary Kamata, Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alidai hawezi kulizungumzia, na alipotafutwa mkurugenzi (Kiomoni Kibamba) kupitia simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa na alipopigiwa tena haikupatikana.

Tangu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, kuanza kuliongoza Jiji hilo, amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na Meya huyo kwa kile kinachotajwa ni maslahi binafsi yanayosababisha mgogoro wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!