Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Manyoni wapigwa msasa
Habari za Siasa

Madiwani Manyoni wapigwa msasa

Geoffrey Mwambe, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni
Spread the love

MADIWANI 28 toka Kata 19 za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wamepatiwa mafunzo maalum ya Uongozi, Maadili na Utawala Bora, Mafunzo, anaandika Dany Tibason.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Aprili 5 hadi 6 Aprili, mwaka huu katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Geoffrey Mwambe akifungua mafunzo hayo amewataka madiwani kuyatumia mafunzo hayo ili yawasaidie katika kusimamia vyema sheria, taratibu na kanuni za utawala bora.

Katika mafunzo hayo pia aliwataka madiwani kujenga ushawishi kwa wananchi katika kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo wilayani humo.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani kumekuwa na baadhi ya waheshimiwa madiwani kutojua mipaka ya utendajikazi wao na kupelekea migongano baina yao na watendaji wa vijiji ndani ya kata wanazozisimamia.

“Hivyo kupitia mafunzo haya, ninaimani yatawasaidia kujua mipaka ya utendaji kazi wao hivyo kwenda kushirikiana vyema na watendaji wa kata na vijiji katika maeneo yaokusimamia shughuli za maendeleo,” amesema Mwambe.

Muwezeshaji wa mafunzo hayo, Stella Saasita ambaye ni mchumi toka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na mbinu za ushawishi madiwani hao, ili kuleta mpokeo chanya kwa wananchi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi hususani miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo, Madiwani walioshiriki mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, wamepongeza uongozi wa halmashauri kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo wameyataja kuwa yenye tija katika kuwaongezea uwezo.

Madiwani hao wamesema mafunzo ambayo wanayapata yatawafanya kuchochea zaidi shughuli za maendeleo katika kata zao pamoja na halmashauri kwa ujumla.

Mbali na hilo kwa pamoja madiwani hao wamesema mafunzo hayo yatawafanya kukua mipaka yao ya kazi na kuondokana na migongano kati ya madiwani na watendaji.

Hata hivyo madiwani wamesema kutokana na mafunzo hayo watawahamasisha wananchi kuchangia shughuliza za maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!