Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Dodoma wamtibua Mtaka, wajiidhinishia milioni 47 za ziara, awagomea
Habari za Siasa

Madiwani Dodoma wamtibua Mtaka, wajiidhinishia milioni 47 za ziara, awagomea

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amegoma kuidhinisha fedha kiasi cha Sh. milioni 47 zilizotakikana kutumiwa na Wakuu wa Idara na Madiwani wa Jiji la Dodoma kwenda mkoani Mbeya kufanya ziara ya kujifunza namna ya uendeshaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya usafi. Anaripoti Danson Kaijage- Dodoma … (endelea)

Akizungumza leo tarehe 20 Oktoba, 2021 katika kikao na watumishi wa Jiji la Dodoma, Mkuu huyo wa Mkoa amesema mbali na gharama hizo, kiujumla ziara hiyo haina tija.

Amesema madiwani 55 waliomba waidhinishiwe bajeti ya Sh milioni 26, watumishi 14 Sh milioni 7.6, usafiri wa kukodi Sh milioni sita na mafuta Sh 5.7.

Amesema madiwani na wakuu hao wa idara walimwandikia barua ya kuomba fedha hizo kwa lengo la kwenda kujifunza kuhusu masuala ya usafi wa mazingira, ukusanyaji wa mapato na namna ya kutokomeza ‘ziro’ mashuleni jambo ambalo amesema linatia shaka.

Amesema wakuu hao wa idara pamoja na madiwani hawakupaswa kufanya hivyo kwani mambo wanayotaka kufuata Mbeya yapo jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa fedha wanazohitaji ni nyingi kiasi kwamba zinatosha kujenga madarasa ya kisasa mawili na kubakisha ziada.

“Hivi kweli uchukue hela za madarasa mawili kwa ajili ya ziara ya kujifunza kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako na unaishi nacho? Dodoma kuna miradi mingapi ya kujifunza hapa, kuna utekelezaji wa miradi mingi unaendelea shida ni uvivu wa kufikiria na si vinginevyo,” amesema.

Amesema kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali ambazo zinatokana na kodi za wananchi masikini huku akiongeza kuwa katika maelekezo ya Ofisi yake, Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma inapaswa kujitafakari kuhusu jambo hilo.

Katika hatua nyingine Mtaka amewatahadharisha watumishi wa Jiji hilo kuacha matumizi ya lugha za hovyo wanapowahudumia wananchi na kusema kuwa hali hiyo inakwamisha juhudi za Serikali katika kumaliza migogoro iliyopo.

Mtaka amesema ili mambo yaende lazima watumishi hao wawe na lugha nzuri kwa wanao wahudumia.

Amesema migogoro mingi ikiwemo ya ardhi inaibuka kila kukicha kutokana na changamoto ya mahusiano mabaya baina ya ofisi nyingi za serikaki na wananchi hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Licha ya hayo ameeleza kuna wakati wananchi wanaonekana kama kero lakini kikwazo kikubwa ni watumishi wenyewe ndiyo tatizo.

“Kuna kipindi tulichukua jukumu la utatuzi wa migogoro ya ardhi, tuliamini ufumbuzi wake umefikia mwisho, lakini hali bado ipo palepale, wapumzisheni wananchi wanaotumia muda mwingi kutafuta suluhu za changamoto zao,” amesema.

Mbali na hayo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri kuongeza ubunifu katika kusikikiza kero za wananchi kwa kujadiliana kwa uhuru ili kumaliza migogoro.

“Hapa mjadala wetu tunafanya ili kumaliza kero za wananchi wa Dodoma “kunguru mwoga huepusha ubawa wake” kika mmoja abaki kwenye nafasi yake, tuweke utamaduni wa kuelezana ukweli” amesema Mtaka.

1 Comment

  • Hongera RC kwa kuzuia ulaji na ubadhirifu. Hata hawaoni aibu? Halafu watakwenda kuomba kura za wananchi – kumbe wanaomba kula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!