Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Madiwani Chamwino watakiwa kuwakumbuka walemavu
Habari Mchanganyiko

Madiwani Chamwino watakiwa kuwakumbuka walemavu

Spread the love

MADIWANI wa Halmashauri ya Chamwino wametakiwa kuhakikisha majengo yanayojengwa yanakuwa na miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa Katibu mkuu Taifa wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Jonas Lubago alipokuwa akizungumza na madiwani hao kwenye warsha ya utetezi wa watu wenye ulemavu wasioona (TLB) iliyofanyika wilayani Chamwino.

Lubago alisema madiwani kwa nafasi zao wanapaswa kuhakikisha wanasimamia majengo ya Umma kwenye kata na halmashauri na kata zao yanawekwa miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu ili na wao waweze kupatiwa huduma za msingi kama wanavopatiwa watu wengine.

“Kinachosikitisha ni kwa kuwa walio wengi madiwani wamekuwa wakitanguliza zaidi siasa zao kwenye masuala ya utekelezaji yanayohusu wanajamii badala ya kuwa wakweli kwenye nafasi zao,” alisema.

Akizungumza kwenye warsha hiyo iliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la The Foundation Civil Association, alisema majengo mengi ya taasisi bado ni changamoto kubwa kwa jamii hiyo ya watu wenye ulemavu.

Wakizungumza kwenye kuchangia kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema kuwa bado kuna changamoto kubwa ya watu wenye ulemavu katika kupata huduma zao za kimsingi kutokana na walio wengi kutothaminiwa na jamii.

Olipa Maganjila diwani viti maalum kata ya Chamwino, aliiomba halmashauri kutoa tamko kuwa majengo yote yanayotoa huduma za kijamii yakiwemo shule za msingi, sekondali na vituo vya afya yanakuwa rafiki kwenye miundombinu yake.

Diwani wa kata ya Buigiri Keneth Yindi, aliomba kuwepo na takwimu sahihi ya watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya vitongoji hadi wilaya ili waweze kuunda umoja utakaowasaidia kupata mikopo lwa ajili ya maendeleo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona wilaya ya Chamwino, Gabriel Masaka, alisema tatizo lililopo kwa madiwani wa halmashauri hiyo kwa watu wenye ulemavu ni kutoshirikishwa kwenye shughuli za kijamii.

Aidha changamoto nyingine pia ni ukosefu wa elimu kwa watu wanaoishi na walemavu hii ikiwa na pamoja na unyanyapaa uliopo wanaofanyiwa na familia wanazoishinazo.

Masaka alisema kuwa kutokana na baadhi ya changamoto hizo bado hata kwenye upande wa serikali itaendelea kuwasahau watu hao na kuwafanya kukosa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu na afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!