Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Chamwino walia uhaba kondomu za kike
Habari za Siasa

Madiwani Chamwino walia uhaba kondomu za kike

Spread the love

 

BAADHI ya madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, wameuomba uongozi wa halmashauri hiyo, usambaze kondom za kike , ili kulilinda kundi hilo na maambukizi ya magonjwa ya zinaa husasan virusi vinavyosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ombi hilo lilitolewa jana tarehe 28 Mei 2021, katika kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo, jijini Dodoma.

Akichangia katika kikao hicho, Mbunge Viti Maalum, Edina Mwachitu ameiomba halmashauri hiyo isambaze kondomu za kike, kama inavyosambaza kondomu za kiume, kwenye maeneo mbalimbali.

“Wanawake walio wengi wanaweza kukaa majumbani kuliko kina baba, ambao baadhi yao ni wanywaji wa pombe na wanaporudi nyumbani wanakuwa wamelewa na hawataki kutumia hizo kondom kwa madai ya wao wanataka waaminiwe tu,”alisema Mwachitu.

Kufuatia maombi hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi katika halmashauri hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Diwani Kenneth Yindi, alikiri uwepo wa changamoto hiyo, akisema kwamba kondomu za kiume peke yake ndiyo husambazwa kwa wananchi.

I’m

Yindi alisema, kuna kila sababu kwa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali, zinazopambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kusambaza kondomu hizo za kike, ili na wao waweze kujilinda na virusi vya ukimwi.

“Tumesikia kilio chenu na halmashauri na taasisi zinginezo zinzojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi, itahakikisha kondomu hizo kwa ajili ya wanawake pia zinasambazwa. Ili waweze kujilinda maambukizi ya virusi hivyo ,”alisema Yindi.

Hata hivyo katika taarifa yake, Yindi alisema halmashauri hiyo mpaka sasa imesambaza jumla ya makasha 10,200 yenye kondomu 508 kila moja, ambayo yamesambazwa kwenye kata z 25 zilizopo ndani ya Wilaya ya Chamwino.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *