June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Madiwani Chadema walazwa korokoroni

Spread the love

ALEXANDER Mnyeti, Mkuu wa Wilaya ya Arusha juzi aliwalaza mahabusu madiwani wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika Mwandishi Wetu.

Madiwani hao wanatoka katika Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru mkoani humo ambapo waliwekwa mahabusu kwa saa 48 katika Kituo cha Polisi cha Usa River.

Waliowekwa mahabusu ni Noah Lembris, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Nuru Ndosi, Happy Gadiel na Winfrida Lukumay.

Sababu za madiwani hao kukamatwa na kuwekwa mahabusu ni madai ya kupotosha umma na kuitukana serikali.

Na kwamba, kazi ya kuitukana serikali pamoja na kupotosha umma imekuwa ikifanywa na madiwani hao kwenye mikutano yao ya kata ndani ya halmashauri hiyo.

Pia mkuu huyo wa wilaya amesema, madiwani hao wamekuwa akifanya ziara na mikutano yao bila kuwa na kibali na kwamba, walipoombwa kibali walishindwa kukabidhi.

Amesema, utaratibu uliotumika na hata kufikia hatua hiyo, waliwaita kwenye kikao cha ulinzi na usalama ambacho yeye ndio mwenyekiti wake na kubaini ziara hiyo kufanywa kinyume na utaratibu.

error: Content is protected !!