Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani Chadema Arusha watawaliwa ‘umalaya’ wa kisiasa
Habari za Siasa

Madiwani Chadema Arusha watawaliwa ‘umalaya’ wa kisiasa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

WIMBI  la  viongozi wa  vyama  vya  upinzani  mkoani   Arusha  kujiuzulu  limeendelea  kushika  kasi  baada  ya  Diwani  wa Viti  maalumu  (CHADEMA ) wilaya  ya  Ngorongoro,  Manda Ngoitika naye   kutangaza  kujiuzulu nafasi  hiyo, anaandika Mwandishi Wetu.

Diwani  huyo  ambaye  pia  ni  Mwanaharakati  anayejihusisha  na  utetezi  wa  kisheria  wa  masuala  ya  wanawake  wa  jamii  za  wafugaji   amesema amefikia  hatua  hiyo  baada  ya  kuona  kuwa hakuna  sababu  ya  kuwa  mpinzani  wakati  yale yote aliyokuwa  anayapinga  sasa  yanafanyiwa  kazi.

Pia  alisema  kuwa  kwa  sasa  licha ya  kuendelea  kukiunga  chama  cha mapinduzi  mkono  na  serikali  yake  anajikita  zaidi  kwenye  shughuli  za  harakati  za  kutetea  jamii  hasa  za  wafugaji  ambazo  bado  zinakabiliwa  na  matatizo  mengi.

“Kulingana  na  sheria  za  sasa  ambazo zinakataza  mtu  kuwa  na  NGO’s  na  pia  kujihusisha  na siasa  nimeona  nianza  kujiimarisha  kwenye  masuala  ya  utetezi  wa  jamii  zaidi “alisema  Manda  Ngoitika -Mwanaharakati.

Amesema  ameona  kuwa  siyo  vizuri  kuendelea  kuwa  mnafiki   wa  kuonyesha  kuwa  yupo  upinzani  wakati  hana  anachopinga  na  kwamba  ameona  ni  bora  awe wazi  na  dunia  ijue  kuwa  sasa  yeye  anaunga  mkono  yanayofanywa  na  serikali  ya  awamu  ya  tano  chini ya Rais  John Pombe  magufuli.

Mkurugenzi  mtendaji  wa  Halmashauri ya  wilaya  ya  Ngorongoro  Raphael Siumbu, amethibitisha  kupokea  barua ya  diwani  huyo.

Naye Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Ngorongoro  Bw, Methew  Siloma  amesema  kiongozi huyo  alitangaza  kujiuzulu  kwenye  Kikao   cha  Baraza  la  Madiwani  mbele  ya  Madiawani  wenzake
Kuhusu  tuhuma  zinazotolewa   za  kuwepo  kwa  ushawishi  wa fedha  wa    kuwafanya  viongozi  hao  kujiuzulu, Siloma  alisema  kuwa  hayana  msingi   kwani  hakuna  mtu  mwenye  pesa  za  kuchezea  na  pia  hakuna  sababu  ya  kufanya  hivyo.

Aidha, Siloma  aliwataka  wanaolalamika  na  kueneza  maneno  ya  kuwepo  kwa  ushawishi  wa fedha  kutambua  kuwa  upepo  wa  kisiasa na  hauzuiliki  na  hata  wanasiasa  wanajua  hivyo   wakubali  matokeo  na  waache  kutafuta  mchawi.

Wimbi  la  madiwani   wa  chadema wa  mkoa  wa  Arusha   kujiuzulu  lilianzia  katika  wilaya ya Arumeru  na  sasa  limekuwa  likieneo  katika  maeneo  mengine  ikiwemo   wilaya  ya  Arusha  . Monduli  na  sasa  Ngorongoro

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!