April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Madiwani CCM wamfurusha mwenzao kikaoni

Spread the love

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamemtimua mwenzao kikaoni kwa kutovaa sare za chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Seleman Segreti, Diwani wa Nyida na wajumbe wengine watatu ndio waliokutwa na mkasa huo baada ya kuelezwa, kukiuka makubaliano ya kuvaa sare za chama hicho, kila wakati panapokuwa na kikao.

Emmanuel Lukanda, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wa Wilaya ya Shinyanga, ndiye aliyesimamia zoezi la kuwatimua wajumbe hao kabla ya kuanza kwa kikao.

Kabla ya kuanza kikao hicho, Lukanda alieleza kushangazwa na hatua ya wajumbe hao kuhudhuria kikao hicho bila kuvaa sare hizo kama walivyokubaliana.

“….hapa naona baadhi yenu hamjavaa sare,” alisema Lukanda na kuongeza “baadaye mtaandika barua za kujieleza kwanini hamkuvaa sare.” Hata hivyo, kikao hicho kiliahirishwa.

Utetezi alioutoa Diwani Segret, alisema hakulala nyumbini kwake kwa kuwa, alikuwa na mgonjwa Shinyanga Mjini, huko ndio alikolala na aliporudi alikwenda moja kwa moja kikaoni.

error: Content is protected !!