Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani CCM, Ukawa waungana kumg’oa M’kiti Halmashauri
Habari za SiasaTangulizi

Madiwani CCM, Ukawa waungana kumg’oa M’kiti Halmashauri

Jengo la Halmashauri ya Ukerewe
Spread the love

HALI si shwari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Mwanza baada ya madiwani 24 kati ya 34 kuandikia na kuisaini barua ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, George Nyamaha, anaandika Moses Mseti.

Uamuzi wa madiwani hao kuandika na kupiga kura ya kutokuwa na imani ni kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na kuingizia hasara halmashauri hiyo zaidi ya Sh. 500 milioni.

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni pamoja na kutafuna fedha za maendeleo Sh. 454 milioni zilizotakiwa kwenda kwenye kata zote za wilaya na Sh. 84 milioni zilizotakiwa kwenda kwenye shule zote za wilaya hiyo lakini fedha hizo hazikwenda licha ya kuidhinishwa na kutolewa.

Nyamaha anatuhumiwa kuteua watu kukusanya mapato ya Halmashauri bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika na kuwapangia vituo vya kukusanya mapato kwa makubaliano ya kuchukua asilimia ya makusanyo, kuingilia  majukumu ya Mkurugenzi (Frank Bahati) kwa kushinikiza kuhamishwa watumishi na kuisababishia hasara halmashauri ya fedha za uhamisho.

Tuhuma nyingine zinazomkabili mwenyekiti huyo, ni kutoa lugha chafu kwa madiwani na kwa watumishi kwa ajili ya kutimiza maslahi yake binafsi, mwenyekiti kuingilia mchakato wa manunizi na kujigeuza bodi ya zabuni na kutumia Sh. 90 milioni kutengeneza madawati bila kufuata sheria ya fedha za kitengo cha manunuzi.

Pia Mwenyekiti Nyamaha, anatuhumiwa kulazimisha kufanyika malipo ya madawati huku madawati yakiwa bado hayajatengenezwa, matumizi mabaya ya gari za halmashauri kwa kuyageuza mali yake kwa kutumia mafuta na kujilipa posho yeye na dereva wake kwa kazi zake binafsi kinyume na taratibu.

Baadhi ya madiwani hao waliokataa kutajwa majina yao waliuambia Mtandao huu, kwamba mwenyekiti huyo amekuwa akiingilia majukumu ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo, kitendo ambacho kinasababisha utendaji duni wa kazi kwa watendaji.

Wamesema kuwa kutokana na ukiukwaji na ufujaji wa fedha za umma, madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na wa upinzani 24 kati ya 34 wameandika na kusaini barua ya kusudio la kumng’oa mwenyekiti huyo.

Wamesema kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali na wa CCM wamekuwa wakimkingia kifua mwenyekiti huyo, pindi madiwani hao wanapokusudia kumg’oa kitendo ambacho kinasababisha kuendelea kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

“Tayari tumewasilisha barua ya ombi la kuitishwa kwa kikao cha baraza la madiwani na madiwani hao wamepiga kura ya kutokuwa na imani na sasa tunachosubiri ni kikao rasmi cha kumg’oa na hatutakubali urasimu huu.

“Mwenyekiti (George Nyamaha) amekuwa akiishinikiza bodi ya zabuni kutoa zabuni kwa upendeleo kwa maslahi yake binafsi bila kufuata taratibu za manunuzi na kikao kisipoitisha tutaangalia hatua nyingine za kuchukua,” amesema Diwani huyo.

Nyamaha alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, amedai suala hilo lipo kwenye kikao na kwamba tuhuma zinazoelekezwa kwake ni kwa sababu ya usimamizi wake wa mapato ya halmashauri hiyo na kumsababishia maadui wengi.

Amesema kuwa katika kikao cha Januari 30, mwaka huu, waliagiza kiasi cha Sh. 451 milioni zinazodaiwa kutafunwa zipelekwe kwenye kata zote na kwamba mpaka sasa ni Sh. 90 milioni pekee zilizoenda kwenye kata tatu.

Nyamaha amesema kuwa kikao kingine cha Machi 17, 2017, kiliidhinisha kiasi cha Sh. 84 milioni kwenda kwenye shule za wilaya hiyo lakini mpaka sasa taarifa zinaeleza kwamba pesa hizo zilitolewa na hazijafika na hazipo tayari zimetafunwa.

“Ukiachilia mbali hizo fedha kuna sh. 32 milioni kwa ajili ya wanafunzi walemavu zilizotolewa na zenyewe zimetafunwa na hiyo yote kuna watumishi wanaohusika na ubadhilifu huo wa fedha wameona wanaenda kuumbuka wameanza kubadilisha maneneo,” amesema Nyamaha.

Frank Bahati, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, alipotafutwa na MwanaHALISI Online, amesema wanaendelea kuchunguza madai hayo na kwamba pindi tuhuma zinazoelekezwa kwa mwenyekiti huyo zitakapothibitishwa kama ni za kweli, taarifa sahihi zitatolewa kwa wananchi.

Hata hivyo, inaelezwa uongozi wa mkoa wa Mwanza na madiwani wanarajiwa kuitisha kikao cha dharura cha kumng’oa mwenyekiti huyo kuanzia sasa kikitarajiwa kuongozwa na Mkuu wa mkoa huo, John Mongella.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!