Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Madini kibao yagundulika Ukanda wa Pwani
Habari Mchanganyiko

Madini kibao yagundulika Ukanda wa Pwani

Aina mbalimbali za madini yanayopatikana Ukanda wa Pwani
Spread the love

SERIKALI imekiri kwamba kwenye Ukanda wa Pwani ya Tanzania kunapatikana madini ya aina mbalimbali ambayo ni barite, chokaa, chumvi, clay, dhahabu, flourite, jasi, kaolin, mchanga, mercury, niobim, ruby, rutile, titanium, zircon na gesi asilia, anaandika Dany Tibason.

Hayo yalielezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medad Kaleman alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rufiji, Mohammed Mchengerwa (CCM) ambalo liliulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM).

Ulega alihoji kuhusina na maeneo mengi ya Pwani huwa na madini mengi, Je, eneo la Rufiji lina madini mengi ili wananchi hao washauriwe ipasavyo kutouza maeneo hayo.

Akijibu, Dk. Kalemani alisema ni kweli kwamba kwenye ukanda wa Pwani wa Tanzania kunapatikana madini ya aina mbalimbali ambayo ni pamoja na barite, chokaa, chumvi, clay, dhahabu, flourite, jasi, kaolin, mchanga, mercury, niobim, ruby, rutile, titanium, zircon na gesi asilia.

Amesema wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kampuni ya Beak Consultants GmbH ya nchini Ujerumani ilifanya utafiti wa awali  kati ya mwaka 2013 na 2014.

‘’Kutokana na utafiti huo madini yaliyobainika katika eneo la Rufiji ni pamoja na chokaa na niobium ambayo hupatikana katika eneo la Luhombero.

Pia alidai kuna viashiria  vya uwepo wa Madini ya barite, dhahabu, flourite, mercury na sulfur katika maeneo ya Wingayongo karibu na Kibiti.

‘’Utafiti wa kina unahitajika ili kubaini kiasi halisi cha mashapo ya madini yaliyopo katika maeneo hayo,’’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!