July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madereva watulizwa kwa kamati ya kudumu

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alipokuwa anazungumza na madereva waliokusanyika kituo cha mabasi Ubungo

Spread the love

HATIMAYE Serikali imetimiza ahadi yake kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ya kuunda kamati shirikishi ya kudumu itakayoshughulikia madai ya madereva yaliyokuwa yakisababisha migomo. Anaripoti Sarafina Lindwino … (endelea).

Makonda katika kujaribu kutuliza mgomo huo, aliomba madereva kuendelea na kazi huku wakiipa muda serikali hadi kufikia leo saa nne asubuhi, iwe imetoa ufumbuzi wa kumaliza tatizo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Makonda amesema serikali imeahidi kumaliza mgogoro huo wa madereva na waajiri wao ndani ya mwezi mmoja, kuanzia tarehe 4 hadi Juni 4 mwaka huu.

Amesema katika kipindi hiki, “imeumdwa kamati maalumu ya kudumu itakayoanza kushughulikia matatizo yao. Kamati hiyo itawashirikisha makatibu wakuu wa wizara tatu za Uchukuzi, Kazi na Ajira na Mambo ya Ndani.”

Wajumbe wengineni wawakilishi watano kutoka kwa madereva, ambao watachaguana wao wenyewe, wakilishi watatu kutoka Darcoboa na wengine watatu kutoka Tatoa.

“Tumefanya hivyo makusudi ili pasionekane kama kuna upendeleo wowote, hivyo kwa kushirikiana na watu wote hao naamini migomo ya madereva itakufa,” amesema Makonda.

Ameeleza kuwa kanuni ya kuwataka madereva kurudi darasani kila wanapokwenda kuhuisha leseni zao limefutwa na kwamba mambo ambayo yataanza kushughulikiwa kwa haraka katika kipindi hicho ni mishahara na posho, bima ya afya na mikataba yao kuandaliwa.

Kwa mujibu wa Makonda, “mikataba hiyo lazima iwe bora na sio bora mikataba.” amesema.

 “Sitegemei tena kuona wananchi wanapata taabu kuhusu masuala ya usafiri, nadhani tatizo limeshaisha. Kuhusu suala la baadhi ya madereva kufukuzwa kazi na waajiri wao, hiyo siwezi kuingilia kwa sababu ni makubaliano yao binafsi,” amesema Makonda.  

error: Content is protected !!