January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madereva kugoma tena Aprili 29

Katibu Mkuu wa Chama cha Madareva Tanzania (TTDA), Rashid Sahel

Katibu Mkuu wa Chama cha Madareva Tanzania (TTDA), Rashid Sahel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu adhima yao ya kukutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Spread the love

UMOJA wa Madereva Tanzania (TTDA), wamepanga kumwandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba akutane nao kusikiliza kilio chao, baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka kupuuza matakwa yao. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).

Katibu Mkuu wa TTDA, Rashid Salehe amesema “tulitaka kuwa na mkutano siku ya kesho, lakini kutokana na siku hiyo kuingiliana na siku kuu ya kitaifa, hatutanya. Badala yake tutafanya Aprili 29 mwaka huu, maeneo ya Kimara Resourt.”

Kwamba, hayo sio maandamano, bali kikao cha kawaida, hivyo jeshi la polisi wasiwawekee hofu. Anaongeza kuwa “usafiri hautakuwepo siku hiyo…tutalaza vyombo”.

Hatua hiyo, imekuja baada ya mgomo wa madereva uliotokea 11 Aprili mwaka huu, wakipinga kanuni mpya zilizopitishwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani za kuwataka kwenda kusoma wakati wa kuhuisha leseni zao.

Kufuatia mgomo huo ulioleta madhara makubwa kwa abiria na uchumi wa nchi,  waziri Kabaka aliwaahidi madereva hao kuwa, suala la kurudi darasani kipengere hicho atakiondoa na kurejesha utaratibu wa zamani na kwamba hawatalipa ada ya Sh.580,000 kama ilivyokuwa imeainishwa.

Pia aliwaambia kuwa, wizara imeanzisha mfuko wa watumishi wanaoumia kazini ambao ni lazima waajiri wao wawalipie ili wafanyakazi wote wanufaike na mfuko huo.

Baada ya makubaliano hayo, Kabaka aliomba kukutana na uongozi wa madereva hao 18 Aprili, ili kujadili suala hilo na wajue jinsi ya kutatua matakwa yao.

Salehe amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, “hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na waziri huyo, hivyo ameendelea kuyapuuza matakwa yetu.”

Amesema, kutokana na hilo, walipanga kuwa na mkutano utakao wajumuisha madereva wote nchini ili kujadili suala hilo.

Kwa mujibu wa Salehe, lengo la mkutano huu ni kuwajuza wenzao kilichojili siku walipokutana na waziri Kabaka ili kuona hatua gani za kuchukua wakati wakisubiri jibu la serikali.

error: Content is protected !!