July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madeni yaitesa ATCL

Ndege mpya  aina ya Bombadier Dash 8-Q400

Spread the love

 

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), limesema changamoto ya mrundikano wa madeni inaathiri utendaji wake na kusababisha lijiendeshe kwa hasraa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, tarehe 30 Julai 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi, katika hafla ya kupokea ndege mpya  aina ya Bombadier Dash 8-Q400, ya shirika hilo,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salam.

Matindi amesema kuwa, madeni hayo yanasababisha ATCL ishindwe kutanua mtandao wake wa safari za kikanda na kimataifa.

“ATCL ina changamoto ambazo zina athiri utendaji na kusababisha hasara,  uwepo wa madeni yaliyorithiwa  athari yake ni kushindwa kuongeza mtandao wa safari na kuongeza hasara ya uendeshaji kutokana na riba huchukuliwa kama gharama ya endeshaji,” amesema Matindi.

Matindi amesema kuwa, changamoto nyingine inayoathiri shirika hilo, ni muundo wake wa umiliki ambao kisheria huifanya kuwa mali ya Serikali.

“Muundo wa umiliki wa ndege ambao kisheria hufanya kuwa mali ya Serikali na hivyo kuhusisha na madeni ya Serikali.  Athari ya muundo huo ni kushindwa kutekeleza utanuzi wa mtandao wa safari wa ATCL. Kutotanua mtandao wa safari  kunaongeza hasara kwa Serikali  kwani matumizi ya ndege yanaendelea kuwa ya chini,” amesema Matindi.

Akijibu malalamiko hayo, Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake imezipokea na kwamba itazifanyia kazi.

“Kwa sababu ya muda nizungumzie kidogo masuala ya changamoto za shirika, kama mlivyomsikia mtendaji mkuu ametaja changamoto,  niwaamabie kwamba changamoto zote tumezipokea na nataka nithibitishe kwamba,  nimepokea mpango kazi wa shirika. Ofisi yangu itapitia kwa kushirikiana na shirika na wizara ili tuone inavyokwenda,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!