June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madansa kuombea amani Tanzania

Spread the love

CHAMA cha muziki wa Disco Tanzania (TDMA) kimeandaa onyesho kubwa la kuombea amani nchini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, litakalofanyika Oktoba 17 mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea).

Kwa mujibu wa Katika mkuu TDMA, Ahsanterabi Mtaki onyesho hilo litafanyika katika ukumbi wa Mikocheni Resort Club kuanzia saa 12 jioni hadi asubuhi.

Mtaki katika taarifa yake hiyo aliyoitoa leo amesema, onyesho hilo ni maalum kwa madansa wa zamani na Madjs wa zamani, ambao wataonyesha vipaji vyao vya hali ya juu vilivyopelekea kuyafanya mashindano ya disko kipindi hicho kuwa juu na kupendwa na watu.

“Tutawaonyesha mabingwa wa disko taifa wa kipindi hicho pamoja na mabingwa wa mikoa, Madjs wakongwe waliokuwa wanakimbiza miaka ya 1990-1980 huko,” amesema Mtaki.

Pia amesema, kutakuwa na madansa wakali mbali mbali kutoka sehemu tofauti kama vile, Bob Banjuni, Jackson, Ommy, Sidgne, Veronica, Black Luba, Bob Kasim, China Lokero na wengine wengi.

Madjs watakaokuwepo ni kama, John Peter, John Bure, Seydu, Catto, Ebony Mwalim, Rach Cut, Masoud Niga na Yong lover.Pia kutakuwa na wasanii waalikwa pamoja na madansa wengine wa muziki wa kizazi kipya na Bongo fleva.

Mbali na hilo amesema, onyesho hilo litafunguliwa na maombi kutoka katika dini zote, huku wagombea ubunge wa mkoa wa Dar es Salaam bila kujali vyama vyao wakialikwa katika onyesho hilo.

error: Content is protected !!