April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Madaktari wapya; JPM atoa masharti

Spread the love

RAIS John Magufuli amemuagiza Kapteni Mstaafu , George Mkuchika,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, kuajiri madaktari wapya 1,000. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 20 Februari 2020, wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya madaktari Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, ametoa masharti kwamba madaktari wanaotakiwa kuajiriwa, ni wale ambao waliokaa zaidi ya miaka mitano bila ajira. kwasasa, madaktari 2,700 hawana ajira nchini.

Kiongozi huyo wa nchi ameagiza madaktari hao watakapoajiriwa, wasambazwe nchi nzima hasa katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa mji.

“Nifahamu tuna madaktari 2,700 bado hawajaajiriwa nitaifanyia kazi, nafikiri tutaanza polepole hata tukaichukua 1000, tuanze na 1,000 mambo yakiwa mazuri tena tuendelea kuajiri. Sababu tuna hospitali vijijini wanahitaji madaktari, na hapa tunaajiri madaktari tu walioahangaika miaka 5. Na wasambazwe vizuri katika mikoa yote,” ameagiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya Dk. Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kumuomba atatue changamoto ya ukosefu wa ajira kwa madaktari, pamoja na kuboresha masilahi yao.

error: Content is protected !!