April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Madaktari wamwangukia Rais Magufuli

Spread the love

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimemuomba Rais John Magufuli kuongeza vibali vya ajira, ili kupunguza wimbi la madaktari wasiokuwa na ajira mitaani, pamoja na kuboresha utoaji huduma za afya nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 20 Februari 2020 na Dk. Elisha Ostai, Rais wa MAT wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya madaktari Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Dk. Osati ameeleza kuwa, madaktari wako tayari kufanya kazi maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi.

“Serikali imeanza na ujenzi, umejenga hospitali. Sasa vyama vya madaktari sisi tuna madaktari vijana wako tayari kufanya kazi maeneo yote mijini na vijijini, wakati ukifika ukitoa nafasi ya kufanya kazi vijana wataenda. Nakutana nao wengi, kwenye hospitali tumejenga na upungufu tulio nao kuongeza vibali vya ajira ili wananchi watanzania sana sana vijinjini waweze kupata huduma vizuri,” amesema Dk. Osati.

Wakati huo huo, Dk. Osati amemuomba Rais Magufuli kutoa motisha kwa madaktari wlaioko maeneo ya vijijini ili kuwatia moyo wasikimbilie maeneo ya mjini.

“Maboreso ya sekta ya afya yawe endelevu, wale wanaofanya kazi vijiji na maeneo ya pembezoni wapewe motisha ili wabaki kule, sisi madaktari baada ya kazi kuna ambao wanabaki kazini, nao wapewe motisha,” amesema Dk. Osati.

Pia, amesema kuna baadhi ya madaktari wakiwemo madaktari bingwa, hawajalipwa mshahara tangu mwezi Desemba mwaka jana.

“Kuna hospitali nyingine watu hawajapewa mishahara tangu mwezi wa 12,  na ni madaktari bingwa sio sawa,” amesema Dk. Osati.

Katika hatua nyingine, Dk. Osati amekemea tabia ya madaktari kunyanyasa wenye kwa wenyewe, huku akieleza kwamba ana taarifa nyingi za malalamiko kutoka kwa madaktari walioko mafunzoni kwamba wananyanyaswa wakati wa mafunzo.

“Imefikia mahali mpaka natamani tuwaapishe madaktari upya, sababu tumekuwa na tabia sio. Tumekwua tunanyanyasana wenyewe kwa wenyewe. Makondata wanatuzidi sana, kama kondakta mwenzie gari imeharibika anamchukua anapata siti anakaa wanaenda vizuri,” amesema Dk. Osati na kuongeza:

“Lakini sisi tunajisahau sana mimi ukija ofisini kwetu  nina taarifa nyingi sana,  madaktari wamekuwa wakinyanyasa wenzao wamepewa, ma intern wawalee,  wenzao wanawanyanyasa, madaktari hii sio sawa.”

error: Content is protected !!