December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madaktari Kenya kugoma tena

Spread the love

MUUNGANO wa Wauguzi nchini Kenya umepanga kufanya mgomo kuanzia leo Jumatatu tarehe 4 Februari 2019 ili kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuwalipa stahiki zao ikiwemo marupu rupu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hii ni mara ya pili kwa muungano huo kuitisha mgomo, ikiwa mara ya kwanza madaktari na wauguzi nchini Kenya mnamo mwezi Novemba 2017 walifanya mgomo, lakini serikali ilifanya mazungumzo nao ndipo wakarejea tena kazini.

 Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi Kenya, Seth Panyako amesema serikali ya Kenya imeshindwa kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa mwezi Novemba 2017 katika kaunti nyingi ikiwemo kaunti ya Nairobi, Kisumu, Taita-Taveta, Kisii, Nyandarua, Elgeyo na Marakwet.

Amesema madaktari na wauguzi katika kaunti hizo hawataripoti kazini hadi pale makubaliano yao na serikali ya mwaka 2017 yatakapotekelezwa.

Kaunti ambazo madaktari na wauguzi wake hawatagoma kutokana na kulipwa stahiki zao ni pamoja na kaunti ya Mombasa, Migori na Machakos.

Hata hivyo serikali ya Kenya kupitia waziri wa Leba, Ukur Yatan amewataka wauguzi hao kusitisha mgomo huo kwa kuwa ameteua kamati itayakayoshughulikia masuala yao na kuandika ripoti ndani ya siku 30.

error: Content is protected !!