January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madaktari bingwa wa figo wahitajika

Daktari Bingwa wa ugonjwa wa figo, Onesmo Kisanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuongeza madaktari bingwa wa magojwa sugu ya figo, kutokana kwamba, umekuwa ni tatizo kubwa moja wapo katika kundi la magojwa yasiyoambukiza, ambayo mchango wake katika kuongeza athari za kiafya na vifo ulimwenguni, unaongezeka siku hadi siku. Anaandika Sarafika Ludwino … (endelea).

Wito huo unakuja zikiwa zimebaki siku chache kufikia maadhimisho ya siku ya Figo duniani, ambayo hufanyika Alhamisi ya pili ya Machi kila mwaka, ambapo shughuli nyingi hufanyika, ikiwemo ya kutoa elimu kwa jamii  juu ya afya na magojwa ya Figo. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Afya ya Figo kwa wote”.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari  Bigwa wa magonjwa ya Figo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jaquline Shoo, amesema serikali inatakiwa kutoa fursa kwa wasomi, kwenda nje ya nchi kusomea magojwa sugu ya figo kutokana na uchache wa wataalamu wa magojwa haya nchini.

Amesema, uchache wa wataalamu wa magojwa sugu ya Figo ni tatizo ambalo linawakabili pamoja na uhaba wa vifaa, dawa na miundombinu ya kuwawezesha kutoa huduma kwa wagojwa hao.

“Kwa mfano mzuri, hapa Muhimbili tupo madaktari bigwa wa magojwa ya Figo watano tu ambao tunatoa huduma. Tunapata wakati mgumu sana ukizingatia vitendea kazi hakuna,” amesema Shoo.

Ameongeza kuwa, takwimu zinaonyesha, asilimia 8 hadi 16 ya watu duniani wameathirika na ugonjwa sugi wa Figo. Kwa mujibu wa wataalamu, hadi kufikia mwaka 2023,  asilimia 70 ya watu  watakuwa wameathirika na ugonjwa huo.

Amefafanua kuwa, utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani, ulibaini kwamba Tanzania inashika nafasi ya 54 katika nchi zinazoongoza kwa vifo vya ugojwa  sugu wa Figo.

error: Content is protected !!