Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madai katiba mpya: Bavicha watuma salamu kwa IGP Sirro
Habari za SiasaTangulizi

Madai katiba mpya: Bavicha watuma salamu kwa IGP Sirro

IGP Simon Sirro
Spread the love

 

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) nchini Tanzania, limemuomba Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo (IGP), Simon Sirro akabidhi pingu wanachama wake, kwani wako tayari kukamatwa kwa ajili ya kupigania katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa katika kongamano la kumbukizi ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, lililoandaliwa na Bavicha na kufanyika leo Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021, makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo, lilishirkisha viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema, ndani na je ya nchi kupitia njia ya mtandao, Mwenyeikiti wa Bavicha, John Pambalu amesema mwkaa ujao wa 2022, utakuwa mwaka wa kupata katiba mpya.

“Mwaka ujao nautangaza mwaka wa mapambano vijana wenye moyo mwepesi ageni mapema. Jambo pekee la kumshauri IGP Sirro atukabidhi pingua na funguo zake wala hatutakimbia Polisi, tutawauliza mnatutakaje? Tutafunga pingu mkono wa kushoto, mkono wa kulia twende, tuko tayari kupigania nchi yetu,” amesema Pambalu.

Mwenyekiti huyo wa Bavicha amewataka vijana ambao hawako tayari katika mapambano hayo, wakae kando.

“Ni wakati wa vijana wasio na wajibu wakae kando. Mwaka ujao tunauita ni mwaka wa mapambano pamoja na mapambano tutakayoongoza kutokea Bavicha, lazima tuwe na mapambano yatakayotokea kila mkoa wa nchi ya Tanzania,” amesema Pambalu na kuongeza.

“Ni wajibu wetu vijana kutafakari wito wetu katika nchi yetu, ni wito wangu kwa vijana wenzangu tutimize wito wetu kudai katiba mpya ndio alama pekee ya kukumbukwa kwamba kuna kizazi Hayati Mwalimu Julius Nyerere alisema nahitaji vijana jeuri dhidi mifumo dhalimu ya nchi, ni wajibu wangu kuongoza baraza la vijana.”

Miongoni mwa watu wanaotarajia kuhutubia kongamano hilo ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika na Kiongozi wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Askofu Emmaus Mwamakula.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!