July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Madada poa’, wateja wao kukiona

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuwakamata wanaojihusisha na biashara ya kujiuza ‘Dada Poa’ pamoja na wateja wanao kwa kuwa si biashara halali, anaandika Happyness Lidwino.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, Simon Sirro, kamisha wa jeshi hilo amesema, hatua hiyo inatokana na kuwa biashara hiyo ni ya kujidhalilisha.

Amesema, kina baba na wazee wengi wamekuwa na tabia ya kuacha familia zao na kuamua kuwafuata wanawake wanaofanya biashara hiyo suala ambalo halileti picha nzuri katika jamii.

“Tunatangaza kiama kwa wanaojiuza pamoja na wateja maana watu wengi wamekuwa wakiacha familia zao na kwenda kununua wanaojiuza, hivyo kuanzia sasa msako mkali unaanza pia tunatoa onyo na watakaobainika watakamatwa,” amesema.

Kamishna Sirro amesema kuwa, sheria ipo wazi na kwamba watawashughulikia vilivyo wanaojihusisha na biashara hiyo kutokana na kuwa ni biashara haramu ambayo haifai hata kuigwa kwenye jamii.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi linamshikilia ‘jambazi’ la Eugine Dominick (29) Mkazi wa Kimara akiwa na silaha aina ya Shot Gun na risasi nne pamoja na baruti migomba sita.

Kamishna Sirro amesema, mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa za kuaminika kwamba, kuna mtu wanayemtilia mashaka ndipo polisi walipofanya ufuatiliajina kumakamata.

Amesema, baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kushiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini na kwamba, upepelezi unaendelea ambapo jalada lake linaandaliwa kupelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DPP).

error: Content is protected !!