June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wachungaji: Magufuli si mwanasiasa

Spread the love

KUWEPO kwa malalamiko kutoka pande nne za nchi kuhusu namna Rais John Magufuli anavyoongoza nchi, kumeliibua kanisa kutoa ombi maalumu kwa viongozi wengine wa dini kumsaidia rais huyo, anaandika Dany Tibason.

Godlisten Daniel, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Nzuguni, Dodoma amewataka viongozi wa dini kumshauri Rais Magufuli ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi na kada zingine.

Hata hivyo amesema, sababu kubwa ya kuwepo kwa malalamiko ni kutokana na yeye (Rais Magufuli) kutokuwa mwanasiasa kwa asilimia 100.

Pia Mchungaji Daniel amesema, katika utawala ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi yake kwa kuzingatia haki na wajibu na asiwepo mtu wa kuonewa.
Akizungumzia utawala wa Rais Magufuli amesema, kwa kipindi kifupi ambacho Magufuli amekuwa rais, kuna mambo ambayo yamezua na sintofahamu hususani katika kisiasa.
Amesema, inaonesha wazi kuwa Rais Magufuli siyo mwanasiasa kwa asilimia kubwa na badala yake ni mtendaji zaidi.

“Kutokana na hali hiyo, watu wengi watashindwa kumuelewa kutokana na misimamo yake lakini wakati huo wanasiasa wengi wanatumia siasa kuficha maovu yao wakiamini kuwa chama kitawakingia kifua.

“Tumeshuhudia utawala uliopita, watu wengi walikimbilia katika siasa kwa lengo la kuficha madhambi yao na sasa imefika hatua kuwa Rais Magufuli kaja na mbinu nyingine, ya kuifanya siasa kutokuwa kichaka cha kujificha na kuficha maovu yao”amesema Mchungaji.

Kuhusu mfumo wa kiutawala amesema, ili nchi iweze kutulia na kila mmoja afurahie matunda ya nchi yake, ni lazima kubadilisha mfumo.

“Mfumo mbovu umesababisha kuwepo kwa watu wengi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na wakati mwingine kila jambo kufanyika kisiasa hata pale isipotakiwa.

“Kila eneo siasa imekuwa ikitawala imefikia hatua ya kuingizwa makanisani na hiyo yote ni kutafuta kichaka cha kuficha maovu,sasa umefika wakati wa kila rahia kujua haki yake na kutimiza wajibu wake,” amesema.
Kuhusu ulipaji wa kodi amesema, ni wajibu wa kila Mtanzania kulipa kodi na ni vyema watanzania wakajenga desturi ya kudai risti pale wanapofanya manunuzi.

 

error: Content is protected !!